Mawaziri wafungwa jela ni Basil Mramba na Daniel Yona.

image

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, imewatia hatiani kwa kukutwa na makosa 10 ya matumizi mabaya ya madaraka na kuwahukumu kifungo cha miaka 3 kila mmoja jela aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Fedha, Basil Mramba, na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja ameachiwa huru bada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake. 

Viongozi hao walikuwa wanakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7/=  kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni iliyopata zabuni ya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini ya M/S Alex Stewart.

Mbali na kifungo hicho cha miaka 3 jela pia Mramba na Yona wanatakiwa kulipa faini ya shilingi mioni 5/= kila mmoja au kwenda jela miaka 2 zaidi. 

Hukumu iliyowatia hatiani ni ya wajumbe wawili kati ya jopo la Mahakimu watatu, ambao ni Jaji Samu Rumanyika aliyeanza kusikiliza kesi hiyo kabla ya kuapishwa kuwa Jaji na Hakimu Mkazi Mkuu Saul Kinemela. 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s