Watch “Maalimu seif Akimkosoa LipumbaJana usiku Makao makuu ya CUF Buguruni” on YouTube

Jana wakati akijiuzulu nafasi ya uenyekiti Wa Wa chama cha CUF, Bw Lipumba alidai kuwa anajiuzulu kwa sababu ya kukiukwa kwa malengo ya #Ukawa ambayo ni kupigania katiba ya wananchi na si kushika dola au kwenda ikulu, kauli hii imezua maswali mbalimbali kutoka kwa wanasiasa na wasomi mbalimbali, wakionyesha kushtuka na kushaangazwa na kauli hiyo kutolewa na mtu aina ya Pro Lipumba, wapo waliokwenda mbali na kusema kuwa hawaamini kama ni kauli yake binafsi Bali mashinikizo kutoka kwa “Watawala” na pia wapo waliosema kauli hii inatokana na ushawishi unaoashiria “kupokea mzigo” lakini wachambuzi mbalimbali wanasema kuwa Prof Lipumba amewageuka wafuasi Wa Upinzani, pamoja na wanachama Wa CUF kwa kuonyesha kujali zaidi maslahi yake na nafsi yake bila kuangalia imani na kujitolea kulikofanywa na wafuasi mbalimbali Wa chama hicho kwa kipindi cha miaka 16 akikiongoza chama hicho, “Lipumba unafahamu wazi kuwa kuna watu wamepoteza Maisha, Mali, na wengine viungo vyao ktk harakati za kukifikisha chama hiki hapa kilipo leo, kitendo cha kujiuzulu kwa sababu za binafsi na kulinda nafsi yke bila kujali wale waliokuwa nyuma yke ni usaliti mkubwa” alisema Mchambuzi mmoja. Na katika kulitambua hilo ni wazi Mh Sharrif Hamad analazimika kutoa kauli ya chama na kuondoa upotoshaji na kauli iliyotolewa na Mh Lipumba kuwa chama cha siasa malengo yake ni kushika dola na si kinyume na hivyo!

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s