Kwa hili hatukubaliani na Magufuli! 

Kwa hili sikubaliani na rais, ni @MagufuliJPM, 

Makala tumeikuta kwa mshirika wetu @mjasirihabari kutokana umuhimu wake nasi tukaona ni vizuri kuiweka hapa ili kuhamasisha na kuufahamisha ulimwengu ndani na nje ya mawazo na michango mbalimbali ya wadau ktk kuijenga Tanzania tuitakayo. Mwanaapolo

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya habari imeripoti kuwa rais amewataka #Mabalozi wanaowakilisha #Tanzania kwenye mataifa mbalimbali ikiwemo #WizarayaMamboNje kutowafuatilia au kujihusisha na Wtznia mbalimbali waliokamatwa kwenye nchi za ng’ambo kwa tuhuma za madawa ya kulevya, kwa mtazamo wangu sikubaliani kabisa na maelekezo haya kwa sbb mbalimbali ambazo nitazitaja hapa. Kwanza ni kwa kutumia maneno ya hekima kuwa mtoto akinyea mkono haukatwi bali unasfishwa, na hapa raisi anasimama kama mzazi ambaye anatakiwa kuusafisha mkono husika na si kuukata. Lakini pia raisi anatakiwa kukumbuka kuwa katiba ni makubaliano ya mkataba baina serikali na wananchi, mkataba ambao yeye ameapa kuulinda kabla hatujampa ridhaa ya kuwa kiongozi, raisi haendeshi wala hatakiwi kufanya maamuzi kwa jinsi anavyoona yeye au kwa jinsi anavyoona hasa ikiwa jambo hilo linahusiana na haki za msingi za watu na mali zao pamoja na uhai, katiba imeweka miongozo na taratibu mbalimbali za kufuatwa. Tunapozungumzia mkataba ni pamoja na jukumu la kumlinda mtzina nje na ndani ya eneo la Tanzania, si hivyo tu kwenye mkataba huo pameanishwa vyombo vya utoaji haki ikiwemo mahakama ambacho ndio chombo cha juu kabisa cha utoaji haki ambacho Wtznia wamekubaliana na serikali yao kutumika ktk jukumu hilo. Hii ina maana Wtznia hawajawahi kutoa idhini hiyo kwa mtu au chombo chochote kingine isipokuwa vile vilivyotajwa ktk katiba ya JMT, kwa muktadha huo kitendo cha raisi kusema kutoa maelekezo kuwa vyombo vya serikali visijihusishe na Wtznia walikamatwa nje ya nchi kwa tuhuma za madawa ya kulevya kwa mtazamo wangu ni kungeuka kwa makubaliano kati ya raisi akiwa mkuu wa dola upande mmoja na wananchi ambao kimsingi ndio #wenyenchi,vitendo hivyi ambavyo vimeendelea kuibuka ktk siku za hivi karibuni mbali na kutengeneza matabaka ya watawala na Watawaliwa bali pia ni kuendelea kukuza mgongano, kutomuaminiana, kumong’onyoa nguzo za utaifa wetu kitu ambacho huko mbele kitakuja kutuletea usumbufu mkubwa na kuathiri nguzo za amani yetu tuliyoijenga kwa muda mrefu na gharama kubwa. Raisi hawezi kusema kuwa Wtznia wakituhumiwa tu tayari ni wahalifu, kutoa kauli hiyo maana yake raisi ameshawahukumu wahusika hata kabla ya mahakama za huko walipo hazijamaliza kazi zake jambo ambalo naamini ni kinyume kabisa na jukumu lake kama raisi la kutulinda kama wananchi wake.

Najua kuna watakaosema kuwa hata huko kuna mahakama na si jukumu la serikali kuingilia mahakama za nchi nyingine, mtazamo huu si sawa na batili kwa sababu zifuatazo, kama nilivyoeleza hapo juu “Tanzania ni nchi huru yenye mamlaka yake kamili hii ni pamoja na vyombo vyake vya utoaji haki, kwa maana si vibaya tukasema kuwa Tanzania haiamini wala serikali haina mamlaka ya kukasimu madaraka ya utoaji haki kwa nchi au mahakama nyingine yeyote ile isipokuwa ile iliyoanishwa ktk katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa lugha nyingine kwakuwa hatuamini vyombo vingine vya utoaji haki isipokuwa nilivyotaja hapo juu. Kwa nukta hiyo ndipo linapokuja jukumu la serikali kufuatilia na ikiwezekana kuwasaidia Wtznia mbalimbali waliokamatwa nje ya nchi kwa tuhuma zozote zile ikiwemo ya madawa ya kulevya. Msingi mwingine wa hoja ya kutokubaliana na raisi ni kwa kutumia akili ya kawaida tu kuwa ulimwengu umebadilika sana kama raisi na wale wote waliowahi kutembea, au wanafuatilia vyombo vya habari wanajua hili, kuna baadhi au wakati vyombo vya dola mahali fulani vinatumika kumbambikia mtu kesi kisha kumfunga au kumnyang’anya mali zake au hata kumdhuru mwili na uhai wake, matukio ya aina hii si ya kutafuta ulimwenguni, kama ndivyo itakuwaje pale ambapo mtzania atafanyiwa kitendo husika na mali, na haki, nafsi ikawa hatarini? Je raisi ana ushahidi gani kuwa Wtznia wote waliokamatwa kwa tuhuma za madawa ya kulevya nchi mbalimbali I kweli kuwa wakijihusisha na si wamebambikwa kesi hizo? Ikiwa hapa nchi tu inaweza kutokea hivyo, kuna ushahidi mbalimbali wa kimazingira na maneno mtaani wa uwepo wa watu ambao wamejikuta matatani na vyombo vya dola kwa kubambikiwa kesi? Mara ngapi tumewasikia viongozi wa juu wakikemea watu wachache ndani ya vyombo vya dola wanaotumia mamlaka yao kuwafungulia watu kesi za uongo na hata kufikia kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu? 

Kwa hili na yanayofanana nayo ushauri wangu kwa raisi, ajue na kufahamu kuwa sisi “wanamitandao” hatupo hapa kuzuia juhudi za kupambana na madawa na uhalifu mwingine bali tupo hapa kuhakikisha juhudi hizo zinafanikiwa na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya amani na maendeleo! Ila juhudi hizo hazitafanikiwa ikiwa hatutafuata sheria, katiba na taratibu za utoaji haki tulizoiwekea!

#kinyumechakesikubalianinarais

Via mjasiriahabari 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s